Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza uongozi wa mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, kusitisha utaratibu wa kuuza mgodi huo kwa mbia mwingine bila kuishirikisha serikali, kwa kisingizio cha kushuka kwa bei ya Almasi katika soko la dunia kutokana na ugonjwa wa Covid 19.
Akizungumza na viongozi na watendaji wa mgodi huo, Biteko amesema kuwa wizara ya Madini haina taarifa zozote za kutaka kuuzwa kwa mgodi huo zaidi ya kuona katika mitandao ya kijamii.
Meneja Mkuu wa mgodi huo wa Almasi wa Mwadui, – Ayoub Mwenda amemweleza Waziri Biteko kuwa hali ya uendeshaji wa mgodi kwa sasa si ya kuridhisha.
