Serikali ya Tanzania yafunga shule kwa siku 30

0
291

Serikali imetangaza kuzifunga kwa muda wa siku 30 shule zote za awali, msingi na sekondari kuanzia hii leo, kufuatia tishio la virusi vya corona.

Akitoa taarifa ya serikali kwa wananchi kuhusu virusi vya corona, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa michezo yote inayokusanya idadi kubwa ya watu ikiwemo ile ya ligi kuu na michezo ya shule, nayo imeahirishwa kwa muda wa mwezi mmoja.

Waziri mkuu amesisitiza kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua za kudhibiti kuingia kwa virusi hivyo nchini na itahakikisha homa hiyo haienei.

Pia amewataka wafanyabishara wote nchini kutotumia kipindi hiki kupandisha bei ya bidhaa zinazotumika kujikinga na virusi hivyo, wa kuwa kwa kufanya hivyo ni kosa.