Serikali kuyafanyia kazi malalamiko kuhusu tozo

0
240

Serikali imesema imesikia na kupokea maoni ya wananchi kuhusu tozo zinazotozwa katika maeneo mbalimbali.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwiguli Nchemba amesema, serikali imeanza kufanyia kazi maoni hayo na itatoa majibu siku za karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi kuhusu tozo mbalimbali, Dkt. Nchemba amewataka wananchi kuwa watulivu wakati jambo hilo linafanyiwa kazi.

Amesema miongoni mwa tozo ambazo serikali inafanyia kazi ni ile ambayo wananchi wanatozwa mara mbili kwenye miamala ya simu na tozo kwenye miamala ya kibenki.

Waziri huyo wa Fedha na Mipango amesema serikali itakaa na wadau mbalimbali na kujadiliana, na kutoka na muafaka ambao utaleta nafuu kwa wananchi.