Serikali kuwasaidia wakulima Mbarali

0
544

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema kuwa serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kuwa wakulima wa wilaya Mbarali mkoani Mbeya ambao ni wakulima wazuri wa Mpunga wananufaika na kilimo hicho.

Waziri Hasunga ametoa kauli hiyo katika uwanja wa Barafu wilayani Mbarali, kabla ya Rais John Magufuli anayeendelea na ziara yake mkoani Mbeya hajazungumza na Wakazi wa wilaya hiyo.