Serikali kutoa tuzo kwa wadau wa sekta ya madini

0
147

Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa madini nchini na katika usiku wa madini kwa mwaka 2021 watakabidhi tuzo 38 kwa wadau waliofanya vizuri kwenye sekta hiyo.

Usiku wa madini utafanyika leo Februari 22, 2021 kuanzia saa 3 usiku na itakuwa mubashara kupitia TBC1

Kaulimbiu ya mwaka huu katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini ni, Sekta ya Madini kwa Uchumi Imara na Maendeleo Endelevu.

Mkutano huo unaendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.