Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amewataka madereva kutii na kufuata kanuni za barabarani katika ubebaji wa mizigo na kutoa wiki mbili kuhakikisha kuwa wale wote wanaodai mpaka wa kasumulu kuanza kulipwa Mara moja kwa sababu pesa ipo na kuagiza wizara ya fedha kuharakisha ulipwaji wa fidia hiyo kufuatia agizo la rais
Aidha Waziri Kamwelwe ameridhia ombi la mkoa wa Mbeya kupata barabara ya bypass mbadala kuepusha ajali za barabara na kuagiza kuanza kwa utekelezaji wa haraka kukamilisha barabara hiyo kiwango Cha changalawe
Waziri Kamwelwe ametoa agizo pia la kuhakikisha wamiliki wa magari ya mizigo watakaokiuka Sheria kwa kuzidisha mzigo magari hayo yatataifishwa hata kama yamebeba mzigo wa serikali