Rais John Magufuli amesema kuwa serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Chama Cha Skauti nchini ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wakati yanapotokea majanga mbalimbali.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kumuapisha Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraji Mnyepe pamoja na Mwantumu Mahiza kuwa Skauti Mkuu wa Tanzania.
Ameongeza kuwa serikali inatambua changamoto mbalmbali zinazokikabili Chama cha Skauti nchini na kwamba itaendelea kuzishughulikia.
Rais Magufuli ameelezea matumaini yake kwa Chama hicho cha Skauti nchini kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kushughulikia masuala mbalimbali chini ya uongozi wa Skauti Mkuu Mwantumu Mahiza.
Kwa upande wa Dkt Mnyepe, Rais Magufuli amemtaka kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kuleta mabadililiko ndani ya wizara hiyo ya Mambo ya Nje na Ushirikikiano wa Afrika Mashariki.
Amesema kuwa wizara hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi, hivyo ni vema akajipanga vizuri ili kuhakikisha anakabiliana na changamoto hizo.