Serikali kushughulia changamoto wanandoa waliotengwa na kazi

0
332

Serikali imesema kuwa inaangalia utaratibu wa kushughulikia suala la wanandoa watumishi wa umma waliotengenishwa kutokana na kazi, ili kuweza kulipatia ufumbuzi bila kuathiri utendaji kazi Serikalini.

“Watumishi wengi wamepangiwa mahala, na wanakwenda kule na harakati za kuanza kuhama tangu siku ya kwanza waliyofika,” amesema hayo Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene.

Ameeleza kuwa wanandoa ambao wametenganishwa na kazi wanapata changamoto ya kutokuwa pamoja lakini pia hawafanyi kazi kwa ufanisi kwa sababu muda mwingi wanawaza mwenza wao wako mbali.

“… tukae na mamlaka za ajira, hasa TAMISEMI, ili tuweze kutengeneza mfumo rafiki,” amesisitiza Waziri Simbachawene

Aidha, ameongeza kuwa pengine watumishi wengine huhama kwa sababu wamepangiwa maeneo ambayo hawayataki, lakini hapo hapo amesisitiza kwamba kumpangia mtumishi eneo alikotoka inaweza isiwe jambo zuri.

Simbachawene amesema hayo akiongezea majibu yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete ambapo alikuwa akijibu swali la Mbunge Hassan Kungu wa Tunduru Kaskazini alilolielekeza TAMISEMI akitaka kujua kuna mpango gani wa kuchukua hatua kwa Watumishi wanaoripoti na kuondoka bila kufanya kazi Wilayani Tunduru.