Serikali kushirikiana na Sekta binafsi

0
100

Serikali imesema itashirikiana na sekta binafsi, ndani na nje ya nchi ili kuongeza kasi ya ujenzi wa miradi ya kimkakati kwa maendeleo ya Taifa, kiuchumi na kijamii.

Hayo yamesemwa jijini Arusha, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Ludovick Nduhiye wakati akifungua semina ya siku mbili iliyoandaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Barabara Tanzania (TARA).

“Kama nchi tuna miradi mingi inayoendelea kutekelezwa hivyo nia yetu ni kuharakisha miradi hiyo kwa kuhusisha pia sekta binafsi hususani kwa miradi ya barabara, madaraja, viwanja vya ndege na miradi mingineyo,” amesisitiza Nduhiye.