Rais John Magufuli ameahidi kuwa Serikali itahakikisha inapeleka kwa haraka miradi ya maji iliyokwama kwa muda mrefu katika jimbo la Singida Mashariki ili Wananchi wa jimbo hilo nao wafaidi kupata uwakilishi wa Mbunge wao mpya.
https://www.youtube.com/watch?v=ktXbBGK9wp8
Akizindua Rada za kuongozea ndege katika uwanja wa wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Rais Magufuli amesema kuwa amefuatilia suala la Mbunge mpya wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu na kwamba serikali itakahakikisha inapeleka miradi ya maji iliyoombwa na Mbunge huyo katika mkutano uliopita wa Bunge.
“Mheshikiwa Spika, nimefurahi kumuona Mheshimiwa Mtaturu hapa na napenda kumuahidi kuwa miradi aliyoiomba inatekelezwa kwa haraka ili wale waliokua hawana Mbunge nao wafaidi kama wengine”, amesema Rais Magufuli.
Miraji Mtaturu ameapishwa kuwa Mbunge wa Singida Mashariki katika mkutano wa 16 wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita, kuchukua nafasi ya Tundu Lissu ambaye Ubunge wake ulitenguliwa na Spika wa Bunge, – Job Ndugai.