Serikali kukamilisha miradi ya maendeleo kwa Wakati

0
145

Rais Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya Watumishi Mkoani Mara kushindwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu licha ya Serikali kutoa fedha, hali inayosababisha kusuasua kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kufuatia hali hiyo pamoja na mambo mengine Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Bunda Vijijini kukaa pembeni ili kupisha uchunguzi kutokana na kutuhumiwa kuhujumu mradi wa ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri hiyo.

“Ndugu Wananchi Serikali pia imeleta milioni mia tano kwaajili ya Ujenzi wa vituo vyao Afya na kwamba vituo hivi havitakamilika, Kuna milioni mia tano zingine za kununua vifaa vitavyohitajika. Lakini pia tumeleta bilioni mia moja na milioni mia nane kwaajili ya Ujenzi wa hospitali ya Wilaya.

Serikali pia imeleta milioni mia tano kwaajili ya wodi ya wakina mama, wodi ya Watoto na akina baba kwenye hospitali iliyopo sasa hivi” ameongeza Rais Samia

Rais Samia anaendelea na ziara ya Kiserikali mkoani Mara ambapo kesho anatarajia kwenda Butiama kuzulu Kaburi la Mwalimu julius Nyerere Pamoja na Kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa chujio la maji mradi wa Maji Bunda