Serikali kujenga meli zaidi

0
155

Rais Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini mikataba mitano ya utekeleza miradi mbalimbali, ambayo ikikamilika itasaidia katika kukuza na kuchochea uchumi wa Taifa.

Mikataba hiyo ambayo imesainiwa wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Mwanza ni ujenzi wa meli mpya katika bahari ya Hindi, ujenzi wa meli ya mizigo katika ziwa Victoria, ujenzi wa meli ya mizigo kwenye ziwa Tanganyika, ujenzi wa meli ya abiria na mizigo katika ziwa Tanganyika na mradi wa ukarabati wa meli ya MV Umoja kwenye  ziwa Victoria.

Utekelezaji wa miradi hiyo unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 430 zikiwa ni fedha za ndani, na fedha hizo zitaanza kutengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/2022.