Serikali kujenga Barabara ya Nachingwea – Masasi

0
170

Rais John Magufuli ameahidi kuwa Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Nachingwea – Masasi, yenye urefu wa Kilomita 45.9.

Akizungumza na Wakazi wa kata ya Naipanga wilayani Nachingwea mkoani Lindi, Rais Magufuli amesema kuwa Serikali itamaliza tatizo la barabara hiyo baada ya kuijenga kwa kiwango cha lami.

Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa na uchapakazi wa Wakazi wa kata ya Naipanga na hivyo kuahidi kuwapa zawadi ya kuwajengea barabara kwa kiwango hicho cha lami.

Mbali na barabara hiyo, Serikali pia itaijenga Barabara ya Nanganga – Ruangwa yenye urefu wa Kilomita 57. 5 kwa kiwango cha lami.