Serikali Kujenga Barabara Ya Ifakara – Mlimba Kwa Kiwango Cha Lami

0
164

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa tatizo la barabara ya kutoka Ifakara hadi Mlimba mkoani Morogoro lililokua likiwakabili Wakazi wa maeneo hayo kwa muda mrefu limepatiwa ufumbuzi, baada ya Serikali kupanga kuijenga kwa kiwango cha lami.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara na Wakazi wa maeneo hayo, mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Matangini, Mlimba wilayani Kilombero, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

https://www.youtube.com/watch?v=k56zzyGkN2U

Amesema kuwa, Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali nchini,  ikiwemo barabara ya kutoka Ifakara hadi Mlimba yenye urefu wa Kilomita 126.5.

 “Serikali imedhamiria kuimarisha barabara katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Ifakara-Mlimba kwa kiwango cha lami,  lengo likiwa ni kurahisisha usafiri pamoja na kukuza uchumi wa Wananchi na Taifa kwa ujumla,” amesisitiza Waziri Mkuu.