Serikali kujenga barabara kuunganisha Serengeti na Mto wa Mbu

0
197

Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara kutoka Makutano – Sanzate – Mugumu hadi Mto wa Mbu ili kuwawezesha Wakazi wa mkoa wa Mara na Arusha kukuza uchumi katika maeneo yao.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Serengeti,- Marwa Rioba, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Elias Kwandikwa amesema kuwa, tayari ujenzi wa barabara hiyo umeanza na ukikamilika utakuwa umefungua fursa kubwa za kiuchumi katika ukanda wa utalii.

https://www.youtube.com/watch?v=u_xElfOuGxg

Mhandisi Kwandikwa amewaambia Wabunge jijini Dodoma kuwa, mbali na barabara hiyo ambayo itafungua zaidi fursa za utalii kati ya wilaya ya Serengeti na Monduli lakini pia itarahisisha usafiri katika maeneo hayo.

Naibu waziri Kwandikwa amesema kuwa, mbali na barabara hiyo, serikali pia ipo katika mchakato wa kuanza ujenzi wa barabara ya Kibaya – Narco – Kiteto – Arusha kwa kiwango cha lami ili kufungua fursa za kiuchumi katika maeneo hayo.