Serikali imesema itahakikisha kuwa usikivu wa matangazo ya TBC Taifa unaimarika nchi nzima kabla ya kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe mara baada ya kuanza ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga yenye lengo la kukagua mitambo ya TBC Mkoani humo .