Serikali kuimarisha ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi

0
122

Serikali kupitia Msajili wa Hazina imekusudia kuongeza ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kutoka shilingi Bilioni 637.64 za hivi sasa hadi kufikia shilingi Trilioni 1.2 mwaka wa fedha wa 2025/2026.

Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu amesema ukusanyaji huo wa mapato unatarajiwa kuongezeka
kutokana na uboreshaji wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato ambayo ni gawio na michango ya aslimia 15.

Mchechu ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam.alipokuwa akizungumza na Wenyeviti wa Bodi pamoja na Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala wa Serikali.

Amesema Serikali imekusudia kuimarisha matumizi ya TEHAMA, ili kuleta ufanisi wa usimamizi na ufuatiliaji wa utendaji wa Taasisi na Mashirika yote ya umma, ili kuwezesha kutekelezwa kwa malengo yaliyokusudiwa.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni Kuimarisha Usimamizi na Uendeshaji wa Taasisi na Mashirika ya Umma kuelekea uwekezaji wenye tija kwa Taifa.