Serikali kuhakiki maombi ya kifuta jasho Nanyumbu

0
146

Serikali imesema itahakiki upya maombi ya kifuta jasho na kifuta machozi kwa Wananchi walioathiriwa na wanyamapori wakali na waharibifu katika halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara ili kuwapatia stahiki zao.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nanyumbu, Ally Mhata aliyetaka kujua idadi ya Wananchi wa jimbo la Nanyumbu ambao wamefidiwa kutokana na uharibifu uliofanywa na tembo katika mashamba yao.

“Nimuombe Mheshimiwa Mbunge kwenye hili suala la takwimu nitazichukua kutoka kwake lakini pia tutaenda kuhakiki upya katika maeneo hayo ili wananchi waweze kulipwa stahili zao.” amesisitiza Naibu Waziri Masanja

Awali, alifafanua kuwa Machi 21 mwaka huu wizara ya Maliasili na Utalii ilifanya malipo ya kifuta jasho ya shilingi Milioni 5.1 kwa wananchi saba wa vijiji vya Michenjeuka, Lukula, Masuguru na Mpombe walioharibiwa mazao yao.