Serikali kugharamia mazishi ya wanafunzi waliofariki kwa moto

0
345

Serikali ya Mkoa wa Kagera imeifunga kwa muda wa wiki moja Shule ya Msingi Byamungu Islamic iliyopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera kufuatia ajali ya moto na kuahidi kugharamia mazishi ya wanafunzi 10 waliopoteza maisha.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema mbali na kutoa gharama za mazishi, serikali itahakikisha wanafunzi wote saba waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu kwa gharama za serikali.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema jeshi la polisi linafanya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo pamoja na kutambua miili ya baadhi ya wanafunzi ambayo imeharibika vibaya.

Wanafunzi wawili kati ya saba waliojeruhiwa ambao hali zao si nzuri huenda wakasafirishwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.