Serikali kuendelea kuwaunga mkono vijana

0
141

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kuwaunga mkono vijana, kuwekeza kwenye miradi itayowakwamua kiuchumi na kuendelea kuwajengea vijana mazingira bora ya kuwekeza nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo mkoani Kagera alipokuwa akizindua wiki ya Taifa ya vijana.

Aidha, amewataka vijana kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kudumisha umoja mshikamano na muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar ili kuendelea kuwa na Taifa imara.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amewapongeza vijana wa mkoa wa Kagera na Tanzania nzima wanaoshiriki katika maonesho ya wiki ya vijana mkoani humo kwa kuendelea kushirikiana vizuri na viongozi wa mkoa huo kuratibu maonesho hayo.

Maonesho hayo ya wiki ya vijana kitaifa yaliyozinduliwa leo na Waziri Mkuu katika viwanja vya Gymkhana, Bukoba yatahitimishwa tarehe 14 mwezi huu, siku ambayo pia ndio itakuwa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru.

Sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa Kaitaba na Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.