Serikali kuendelea kutoa Elimu bora

0
177

Serikali imeahidi kuendelea kutoa Elimu Bora kwa Wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuimarisha shule kongwe na vyuo vya Elimu ya juu nchini.

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika kipindi cha miaka minne ya utawala wake.

Dkt Abbasi amesema kuwa, kuna ongezeko la Wanafunzi Milioni moja baada ya kuanza kutolewa kwa Elimu bure, na hivyo Serikali inafahamu changamoto inayojitoleza na tayari imeanza kufanya ukarabati katika shule kongwe na kujenga mabweni zaidi ya 500 kwenye Vyuo Vikuu mbalimbali hapa nchini.

Msemaji Mkuu huyo wa Serikali ameongeza kuwa, zaidi ya Shilingi Bilioni 70 zimetengwa na Serikali kwa ajili ya kukarabati shule kongwe ili ziweze kuchukua Wanafunzi wanaomaliza kidato cha Nne.