Serikali kuendelea kushirikiana na wadau wa Madini

0
174

Waziri wa Madini Dotto Biteko amewataka wadau kwenye sekta ya Madini kushirikiana na Wizara ya madini ili kuboresha sekta hiyo na kuahidi kufanyia kazi ushauri na mapendekezo ya wadau.

Katika Mkutano huo ambao umeshirikisha nchi 11 za ukanda wa maziwa makuu Waziri Biteko amesema lengo la Mkutano huo ni kuwashirikisha wadau ili kuhakikisha watu wote wananufaika na sekta ya madini katika njia na mipito ambayo ni sahihi na kueleza kuwa kwa sasa watanzania wanafaidika na madini na sio kutumika kama manamba.