Serikali kuendelea kushirikiana na wadau sekta ya madini

0
187

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya madini ili kuongeza tija na pato la Taifa

Makamu wa Rais amezungumza hayo leo wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya Madini unaofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais amemtaka Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhakikisha anatatua na kushughulikia changamoto zilizopo katika sekta hiyo.

Mkutano huo unatarajiwa kumalizika kesho huku wadau mbalimbali katika sekta ya madini wakipata fursa ya kuonesha bidhaa zao katika mabanda yaliyopo katika ukumbi huo.