Serikali kuendelea kukuza sekta ya Utalii

0
205

Serikali imesema kuwa inaendelea kufanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha Sekta ya utalii inakua na inatoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla wakati wa ufunguzi wa onesho la Kiswahili la Utalii la Kimataifa (SITE) kwa mwaka 2019.

Amesema kuwa miongoni mwa jitihada hizo ni kuboresha miundombinu katika maeneo mbalimbali ya utalii, ikiwa ni pamoja na ile ya barabara ili kuwawezesha Watalii wengi kufika katika maeneo hayo.

Mkutano huo wa SITE kwa mwaka huu yanahudhuriwa na Wadau wa masuala ya Utalii kutoka ndani na nje ya nchi.

Wakati wa mkutano huo, kunafanyika pia maonesho mbalimbali yanayohusu Sekta Utalii.