Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Augustine Mahiga amesema kuwa serikali inaendelea kukagua mikataba yote mipya ya wawekezaji nchini ili kuhakikisha mikataba hiyo inaleta tija kwa Taifa.
Akijibu swali bungeni jijini Dodoma, Waziri Mahiga amesema kuwa hivi sasa kila wizara na kila sekta zimekuwa zikipeleka rasimu za mikataba mipya ya wawekezaji kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa ajili ya uhakiki.