Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya kilimo kwa vijana

0
98

Serikali imeandaa mpango wa Kampeni ya Kilimo Ajira kwa vijana ikiwa ni sehemu ya matumizi ya bajeti ya mwaka huu wa fedha ya shilingi bilioni 954 katika kuongeza ajira kwa vijana kupitia sekta ya kilimo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde wakati akifanya mahojiano na Mtendaji Mkuu wa Africa Media Group Limited, Shaaban Kisu kuhusu mpango huo.

Mavunde amesema kupitia mpango huo Serikali inapima mashamba, rutuba ya udongo, kuwatafutia mbegu na pembejeo na kuwatafutia masoko ili kuwezesha kilimo ajira Kwa vijana.

“Katika bajeti yetu ya mwaka huu tumepata ongezeko kubwa la fedha kutoka shilingi bilioni 294 mpaka shilingi bilioni 954 na katika mkakati mmoja wapo tulionao ni kuhakikisha sisi kama wizara tunasaidia kutatua hili tatizo la ajira hasa kwa vijana na tunalifanya hilo kupitia sekta ya kilimo,” ameongeza Mavunde

Katika mazungumzo hayo Shaaban Kissu amewataka vijana kuchangamkia fursa hiyo ambayo ni suluhisho la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini.