Serikali kuendelea kuboresha Jeshi la Zimamoto

0
158

Serikali imejipanga kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ikiwa ni pamoja na kutoa maslahi mazuri kwa watendaji wa jeshi hilo na kuboresha mazingira ya kazi.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ufunguzi wa jengo la Zimamoto na Uokoaji lililopo wilayani Temeke.

Amesema Serikali inakwenda kulifanya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuwa la kisasa kwa kuwekeza fedha zaidi ili liwe bora zaidi.

Aidha, Waziri Masauni amesema Serikali itaendelea kujenga vituo vya zimamoto na uokoaji nchini, lengo likiwa ni kuendelea kuboresha huduma zinazotolewa na jeshi hilo kwa Wananchi.