Serikali kuendelea kuboresha huduma za TTCL

0
206

Serikali imesema itaendelea kuwekeza fedha za kutosha kwa ajili ya Shirika la mawasiliano Tanzania (TTCL) ili kufanikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi wake popote walipo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Jim Yonaz wakati wa mkutano wa baraza la Wafanyakazi wa TTCL uilofanyika Jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo Dkt.Yonaz amesema Shirika la mawasiliano Tanzania (TTCL) ni moja mashirika muhumu yanayotegemewa na Serikali kuwafikishia wananchi wake huduma ya Mawasiliano na hivyo kuwataka watendaji kufanya tafiti nyingi zenye kuleta matokea chanya.

Kwa Upande wake Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Waziri Waziri Kindamba ameeleza namna walivyojipanga kushirikiana na shirika la Umeme nchini TANESCO katika kuwafikishia wananchi huduma ya Mawasiliano popote walipo.