Serikali kudhibiti picha chafu mtandaoni

0
133

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeongeza uwekezaji katika teknolojia ya udhibiti wa picha zisizofaa kwa wananchi.

Waziri Nape amesema hivi karibuni TCRA itakuja na mpango maalum wa kudhibiti picha chafu mtandaoni na pia kufuatilia wale wote wanaosambaza picha hizo.

Akijibu swali la Mbunge wa jimbo Kinondoni, Abbas Tarimba aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali katika kudhibiti picha chafu mtandaoni kama nchi zilizoendelea, Waziri Nape amesema kwa sasa TCRA inafunga mitambo ya kudhibiti picha hizo kwa watumiaji wa mitandao hapa nchini.