Serikali Kuajiri Wataalamu 550 Wa Afya

0
234

Serikali ipo katika mchakato wa mwisho wa kuajiri Wataalamu 550 wa afya ambao watapelekwa kwenye vituo vya afya, hospitali na zahatani nchi nzima, ikiwa ni hatua ya kupunguza tatizo la uhaba wa Wataalamu wa afya nchini.

https://www.youtube.com/watch?v=JgySxfaRwp0

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), -Josephat Kandege wakati akijibu maswali ya nyongeza ya Mbunge wa Ukerewe,- Joseph Makundi na Mbunge wa Rombo,- Joseph Selasini waliotaka kujua namna Serikali ilivyojipanga kukabiliana na uhaba wa Wataalamu wa afya hapa nchini.

Akijibu maswali ya Wabunge hao, Naibu Waziri Kandege amesema kuwa, katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 Serikali imepanga kuajiri watoa huduma za afya 550 ambao watapelekwa kwenye vituo vya afya na zahanati kote nchini.

Aidha Naibu Waziri Kandege amesema kuwa, msisitizo utawekwa kwenye maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi ikiwa ni pamoja na visiwa vya Ukerewe na maeneo mengine ya pembezoni.