Serikali ina dhamira ya kurekebisha sheria ya mirathi

0
235

SHIRIKA la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WilDAF) limesema kuwa Serikali inaendelea kufanyia marekebisho ya  sheria mirathi ili kuweza kutoa haki kwa wajane pindi wanapokuwa wamefungua shauri linalohusiana na mirathi.

Akizungumza na  TBC kuelekea kilele cha siku wajane Duniani Mwanasheria wa Sherika hilo Zakia Msangi amesema kuwa serikali imekuwa karibu katika kuhakikisha maboresho ya sheria ya mirathi kwa wajane  inaboreshwa na kazi hiyo wameendelea kuifanya kuweza kupata maboresho hayo.

Amesema kumekuwa na  majadiliano ya wadau mbalimbali wanaoagazia  masuala ya sheria ya wajane ,watoto ambapo serikali imekuwa ikishiriki kwa kuchukua mawazo katika kuweza kufanya maboresho ya sheria hizo.

“Tumeona dhamira ya serikali katika kufanyia marekebisho sheria ya mirathi  hii itatoa haki kwa wajane ambapo ni tofauti na ilivyo kwa sasa kwani wajane wengi hawajui hata namna ya kuweza kufungua shauri la mirathi katika mahakama”amesema Msangi.

Ameongeza katika maboresho juu kuwepo kwa adhabu ya wafujaji mali za marehmu ili kuweza kuwa fundisho kwa wengine wanaokimbilia mali huku wakiacha wajane wakiteseka.

Nae Mkurugenzi wa Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) Rose Sarwatt amesema katika maadhimisho hayo kufanya ni mara sita na kuwa na mwitikio mkubwa wanawake wajane katika kufikisha kilio chao katika masuala yanayowazunguka.

Amesema kuwa wana ofisi katika kila kanda ambapo wajane wengi wamekuwa na changamoto katika mirathi kutokana na mila na desturi ya wanawake kutopewa kipaombele pindi anapoondokewa na mwenza wake.

Mjane Faith Mwansye-Okoyo amaesema amesema wajane wanapitia katika changamoto kubwa pindi ndugu wa  marehemu wanapofika katika kuhakikisha wanamiliki mali bila kujua hata mahitaji ya watoto.

Amesema kuwa katika suala muhimu ni kuwa na Utamaduni wa kuandika wosia kwa pande zote hali ambayo itapunguza dhuruma za mali za marehemu.