Serikali: Faragha kwa wafungwa na wenza wao bado

0
174

Serikali imesema bado inaangalia uwezekano wa kuweka mazingira mazuri ya kutoa fursa kwa wafungwa kuwa na faragha na wenzao wao wakati wakitumikia adhabu zao gerezani.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Masauni Hamad Masauni amesema, kwa sasa wizara yake inaangalia namna bora ya kutoa haki hiyo kwa wafungwa lakini ni lazima uandaliwe utaratibu mzuri wa kutoa faragha hiyo.

Waziri Masauni amesema, tendo la ndoa ni faragha ambayo inapaswa kuwekewa mazingira mazuri, ili kuwe na staha kwa wanaohitaji fursa hiyo.

Hata hivyo Mhandisi Masauni amesema, tendo la ndoa sio haki ya msingi ya mfungwa.