Sekta ya maji na nishati kumuinua mtoto wa kike kiuchumi

0
152

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezaeshaji Wananchi Kichumi, Beng’i Issa amesema Serikali imejielekeza kumwinua mwanamke hususani mtoto wa kike kiuchumi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya maji na nishati nakuleta matokea chanya kwenye jamii.

Beng’i ametoa kauli hiyo wakati akizindua jarida la wanawake mkoani Dar es Salaam liloandaliwa na Taasisi ya Purple Planet kwa lengo la kuwainua wanawake kiuchumi kupitia majarida ya wanawake.

Aidha, Beng’i amebainsha kuwa kutengenezwa kwa jarida hilo kutakuwa msaada mkubwa katika kujifunza mambo mbalimbali yenye tija kwenye jamii ikiwa ni pamoja na kutunza kumbukumbu za msingi.

“Mafano kama huu wa kutengeneza jarida unatuwezesha kujifunza lakini pia kutunza kumbukumbu ya yale yaliyoandikwa kwa ajili ya kizazi kijacho,” amesema Beng’i Issa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Purple Planet, Hilda Kisoka amesema jarida hilo litaisadia kwa kiasi kikubwa kufikisha taarifa muhumu kwa wanawake ikiwemo kujua fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye jamii.

Uzinduzi wa jarida hilo imekwenda sambamba na utoaji wa vyeti kwa washiriki wapatao 10 ambao wamefanikisha kuandaa maudhui yaliyochapishwa katika jarida hilo.