Samia kuzindua ‘Tamasha la Urithi’

0
2020

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais Dkt.John Magufuli anatarajiwa kuzindua maadhimisho ya Tamasha la Urithi la Kitaifa jijini Dodoma, linaloandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dodoma Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge amesema tamasha hilo linalenga kuongeza vivutio vya utalii ikiwa ni pamoja na mazao ya utamaduni na mali kale.

Dkt Mahenge amewataka wananchi wa Dodoma na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya taifa Audax Mabula amesema tamasha hilo litasadia kuongeza Watalii nchini.