Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza atatoa shilingi milioni tano kwa kila goli litakalofungwa na timu za Simba na Yanga kwenye michuano ya klabu barani Afrika.
Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.
Simba inacheza michuano ya ligi ya mabingwa Afrika na Jumamosi wiki hii inashuka dimbani kumenyana na Raja Casablanca ya Morocco mchezo utakaochezwa kwenye dimba la Mkapa, Dar es Salaam saa moja jioni.
Yanga wao wapo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho na Jumapili wiki hii watashuka kwenye dimba la Mkapa kumenyana na TP Mazembe ya DR Congo.
Ikumbukwe timu zote mbili zimeanza vibaya hatua ya makundi ya mashindano hayo ya CAF Simba wakifungwa 1-0 na Horoya huku Yanga wakipoteza 2-0 mbele ya US Monastir.