Salamu za pole zimeendelea kutolewa kwa familia ndugu, jamaa na marafiki wa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Mzee Reginald Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia hii leo huko Dubai.
Miongoni mwa salamu hizo ni zile za kutoka kwa Rais John Magufuli ambaye katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter ameelezea kupokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mzee Mengi.
Amesema kuwa Mzee Mengi atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya Taifa na katika kuyasaidia makundi mbalimbali ya kijamii.
Mzee Mengi alikua ni miongoni mwa Wafanyabiashara wakubwa hapa nchini.