Safari za baharini zarejea

0
166

Mamlaka za Zanzibar zimerejesha safari za baharini baada ya kuzisitisha kuanzia Aprili 24, 2021 asubuhi ikiwa ni tahadhari dhidi ya Kimbunga Jobo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kueleza kuwa kimbunga hicho hakipo tena nchini, hivyo hakuna athari zozote za moja kwa moja zinazoweza kutokea.