SADC PF Kuangazia masuala ya chakula

0
116

Rais wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC PF 53) Roger Mancienne amesema, jukwaa hilo litaendelea kuangazia masuala ya uhaba wa chakula na kuzishauri nchi Wanachama namna ya kukabiliana na tatizo hilo.

Mancienne ambaye pia ni Spika wa Bunge la Seychellea amesema, Tanzania imeonesha njia ya kukabiliana na tatizo hilo kwa kuanzisha kilimo cha kisasa kinachohusisha vijana na njia za umwagiliaji, ili kujihakikishia uhakika wa chakula muda wote.

Akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano huo wa 53 wa Jukwaa la Mabunge ya SADC Mancienne amesema, SADC PF itaendelea kuzishauri Serikali za nchi hizo kujifunza kutoka kwenye nchi nyingine ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa chakula.