Sabasaba 2022

0
154

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha ametembelea mabanda ya wafanyabiashara na taasisi mbalimbali yaliyopo ndani ya banda la wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar ambalo lipo ndani ya viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam.

Miongoni mwa mabanda aliyoyatembelea ni la Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Zanzibar (ZURA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) na Viwanda vya Idara Maalum Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Leo ni siku ya tatu ya maonesho ya 46 ya biashara ya kimataifa, Sabasaba, 2022.