Sababu za Vifo vya Majeruhi wa Ajali ya Moto

0
193

Daktari Bingwa wa Upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam Edwin Mrema amesema kuwa, kuongezeka kwa vifo vya majeruhi wa ajali ya lori la mafuta iliyotokea tarehe 10 mwezi huu mkoani Morogoro ni kutokana na kuungua kwa miili yao kwa zaidi ya asilimia Sabini.


Dkt MREMA amewaambia Waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa, kuungua moto kwa asilimia kubwa ndani na nje ya miili yao, kumepoteza kinga ya mwili kujilinda dhidi wadudu .

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, -Aminiel Eligaesha amesema kuwa, vifo vya majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa hospitalini hapo, havitokani na hospitali hiyo kukosa Wataalamu na vifaa tiba kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu .

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali hiyo ya moto iliyotokea mkoani Morogoro imefikia Mia Moja