Sababu ya uzinduzi wa Royal Tour kuanzia Arusha

0
226

Arusha kuwa kitovu cha utalii nchini Tanzania ndio sababu ya kuchaguliwa kuwa sehemu ya kwanza kuzindua filamu ya The Royal Tour inayotazamiwa kukuza utalii na uwekezaji.

Siri hiyo imefichuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza kwa ufupi na wadau  wa utalii waliofika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), kushuhudia uzinduzi wa Tanzania: The Royal Tour.

Amesema baada ya Arusha sehemu y pili kwa utalii ni Zanzibar, Mei 7 mwaka huu, na Mei 8 ni Dar es Salaam, jiji la kibiashara Tanzania.