Sababu ya kutumbuliwa kigogo TPA

0
220

Mapema leo Rais Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Kipande cha nne (Tabora – Isaka) ameeleza kusikitishwa na utendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) tamko lililofuatiwa na kutenguliwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo.

Rais Samia ameeleza umuhimu wa bandari ya Dar es Salaam ikiwemo kuiunganisha Tanzania na nchi za Asia na Afrika na kuwataka wote waliokabidhiwa majukumu ya kufanya kazi bandarini kuongeza jitihada katika kazi zao.

“ Siridhishwi kabisa na kasi za bandari, siasa zilizopo, longolongo zilizopo,” ameeleza Rais Samia.

Aidha, amesisitiza kuwa kama bandari itafanya kazi kama inavyopaswa nusu ya bajeti ya kila mwaka itatoka ndani ya bandari ya Dar es Salaam.