Saba wanusurika kifo Iringa

0
159

Watu saba wamenusurika kifo baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso kwenye ajali iliyohusisha gari la wagonjwa katika eneo la Ilula, Kilolo kwenye barabara kuu ya Iringa – Dar es salaam.

Ajali hiyo iliyotokea majira ya mchana na kuhusisha lori la mizigo lenye shehena ya shaba likitokea nchini Zambia na gari la wagonjwa la mkoa wa Njombe ilisababisha adha ya usafiri kwa takribani saa mbili baada ya lori hilo kuziba barabara hiyo inayotegemewa kwa usafiri wa ndani na nje ya nchi.

Mkuu wa mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amefika eneo la tukio na kuzungumza na manusura huku majeruhi mmoja akikimbizwa Hospitali kwa matibabu.

Sendiga amelitaka jeshi la polisi kuendelea kutoa leimu kwa madereva kuacha kuendesha kwa mwendo kasi na kuhatarisha maisha yao.

Jitihada za vyombo la usalama zimesaidia kusogeza magari yote mawili na safari kuendelea kama kawaida.