Rwegasira Naibu Meya Kinondoni

0
148

Rwegasira Joseph amechaguliwa kuwa Naibu Meya wa manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, baada ya aliyekuwa akishikilia kiti hicho kumaliza muda wake.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi, mwenyekiti wa kikao cha uchaguzi huo Katibu Tawala wa wilaya ya Kinondoni, Stela Msofe amesema waliopiga kura ni madiwani 25, ambao wote wamempa Rwegasira kura za ndio.

Rwegasira amewashukuru madiwani hao wa Kinondoni kwa kumpa kura zote za ndio, na amewaahidi ushirikiano.