Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imetoa onyo kwa Vyombo vya Habari vinne ikiwemo Efm Radio na Dizzim Online kwa kukiuka kanuni za Utangazaji ya maudhui ya radio na Televisheni ya Mwaka 2018.
Akitoa hukumu hiyo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Habbi Gunze, amesema kuwa maudhui hayo yalirushwa na vituo hivyo kwa nyakati tofauti ambapo Dizzim Online kupitia kipindi Cha Joint Mtangazaji wake Salam maarufu SK alionekana akivuta Sigara akiwa anafanya mahojiano na Ritha Paulsen bila kuweka alama ya tahadhari kwa hadhira.
Aidha Dizzim Online imepigwa faini ya shilingi laki tano huku ikitakiwa kutoa mafunzo kwa watangazaji wake ili kuepusha makosa yasiyokuwa na tija wakati wa kuzalisha vipindi vyao ambapo kituo cha Efm Radio imepewa onyo na faini ya shilingi milioni moja ambazo wanatakiwa kuzilipa ndani ya siku ishirini na moja tangu kutolewa kwa adhabu hiyo.
Vyombo vingine vilivyopewa adhabu na mamlaka hiyo nakuonywa ni pamoja na Times FM Radio na DINA MARIOS BABY COCONUT OIL ONLINE TV
Pamoja na mambo mengine Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeweka wazi rufaa kwa vyombo vyote vilivyopewa adhabu hiyo.