Rungu la Serikali kwa Gazeti Gazeti la Uhuru

0
166

Serikali Kupitiai idara ya Habari Maelezo imesitisha kwa siku kumi na nne (14) leseni ya uchapishaji na usambazaji wa Gazeti la Uhuru kuanzia kesho Agosti 12, 2021 baada ya kubaini Mapungu ya kisheria na weledi Katika taaluma ya uandishi wa Habari.

Taarifa ya Idara ya Habari MAELEZO iliyosainiwa na Mkurugenzi wake Gerson Msigwa imeeleza hautua hiyo imechukuliwa baada gazeti la Uhuru kuchapisha Habari yenye kichwa kichwa kinachosema “Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa hana mpango wa kugombea urais 2025”.

“Ofisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maelezo, imebaini kuwa habari hiyo ina upungufu wa kisheria na weledi wa taaluma ya Uandishi wa Habari kwa kutoa taarifa ya uongo dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kinyume na kifungu cha 50(1)(a),(b), na (d) na kifungu cha 52(d) na (e) vya Sheria ya Huduma za Habari Na.12 ya 2016.

Taarifa hiyo imesema Rais Samia Suluhu Hassan hajatoa matamshi yoyote ambayo yanaeleza kutokua na wazo la kuwania urais mwaka 2025

Taarifa hiyo imetoa nafasi kwa Gazeti la Uhuru kukata rufaa kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kiwa hawajaridhika na adhabu hiyo kama ambavyo inaelezwa katika kifungu cha 10 (1) cha Sheria ya Huduma za Habari Na.12 ya 2016.

Aidha Taarifa hiyo imewakumbusha waandishi wa Habari kuzingatia sheria, maadili, kanuni na miongozo mbalimbali inayohusu tasnia ya Habari Ili kulinda taaluma na ustawi wa jamii.