Rungu la NEMC lazishukia kampuni za mafuta

0
138

  Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) limezipiga faini kampuni 9 za mafuta, kwa kosa la kuendesha shughuli zao bila kuwa na cheti cha tathmini ya mazingira.
 
Hatua hiyo ya NEMC inafanya jumla ya kampuni zilizopigwa faini kwa kosa hilo kufikia kumi, huku kampuni hizo zikitakiwa kulipa faini hizo ndani ya siku saba kabla ya kuchukuliwa kwa hatua zaidi.
 
Mkuruggenzi Mkuu wa NEMC Samuel Gwamaka amewaeleza waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuwa, ukaguzi uliofanywa na Baraza hilo umebaini vituo vya mafuta 393 vinavyomilikiwa na kampuni mbalimbali nchini vinaendeshwa bila kuwa na cheti cha tathmini ya mazingira huku vikijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
 
 Dkt. Gwamaka amesema ukaguzi huo ni endelevu, na hivyo kuzitaka kampuni zote kuhakikisha zinakuwa na cheti cha tathmini ya mazingira.
 
Ameitaja mikoa ambayo imekuwa na vituo vya mafuta ambavyo havijakidhi matakwa ya kisheria kuwa ni Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro, Kigoma na Kagera.