Rudiger kukunja mkwanja mrefu Real Madrid

0
141

Ikiwa dili lake litakamilika kujiunga na kikosi cha Real Madrid akitokea klabu ya Chelsea basi beki Antonio Rudiger atakunja mkwanja mrefu.

Rudiger anatarajiwa kuondoka kwenye kikosi hicho na timu kadhaa Ulaya zinatajwa kuwania saini yake.

Ambao wapo mbele kuwania saini yake ni Real Madrid ambao wao wametenga kabisa kitita cha mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki.

Ni mara ya pili tayari Madrid wamepeleka ofa kwa ajili ya kumpata beki huyo lakini wamekutana na kizingiti kutoka kwa PSG na Bayern Munich ambao nao pia wanawania saini ya beki huyo.

Beki hyuyo mwenye miaka 28 mkataba wake ndani ya Chelsea umebakiza miezi sita na Chelsea nao pia wanahitaji huduma yake.