Rosemary Nyerere azikwa

0
244

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo ameshiriki mazishi ya mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, – Rosemary Nyerere aliyefariki dunia Januari Mosi mwaka huu jijini Dar es salaam.
 
Mazishi hayo ya Rosemary Nyerere yamefanyika katika makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo kwenye Kituo cha Hija kilichoko Pugu jijini Dar es salaam.
 
Ibada ya mazishi ya Rosemary imeongozwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Immaculata lililopo Upanga jijini Dar es Salaam, -Dias Mario.
 
Viongozi wengine walioshiriki katika mazishi hayo ni pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Mama Sitti Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba
 
Wengine ni mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,
Spika Mstaafu wa Bunge,- Anne Makinda na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Aboubakary Kunenge.

Rosemary ameacha Watoto Watano na Wajukuu watatu.