Ripoti ya CAG kukabidhiwa kwa PAC na LAAC

0
186

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema ataikabidhi ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kamati mbili za Bunge.

Spika Ndugai amezitaja kamati hizo kuwa ni Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).

Ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma muda mfupi baada ya Serikali kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa hesabu za Wizara, Taasisi na Mashirika yaliyo chini yao.

Taarifa za ukaguzi wa hesabu zilizowasilishwa ni pamoja na ile ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora.